Sunday, June 28, 2009

Fainali za Confederation

Cup 2009. Hata Marekani

wanacheza soka

Brazil vs. Marekani 3 - 2



Mpira ulianza saa 20.35 na filimbi ya

kumaliza mechi saa 22.24 CET

Marekani walianza kwa kucheza ”total football” aliwabana Brazil kuanzia filimbi ya kuanza mpira ilipopulizwa na walifanikiwa kufunga goli la kwanza dakika ya 10 lililofungwa na Clint Dempsey. Dakika ya 27 Brazil walifanya kosa wakiwa kwenye goli la Marekani kwa kupeana pasi mbovu na Marekani walitumia nafasi hiyo kufanya ”counter attack” na Landon Donovan alifunga goli la pili kwa Marekani. Brazil walijitahidi weee..lakini wapi. Hadi mapumziko Marekani walikuwa wanaongoza kwa magoli mawili

Baada ya mapumziko Brazil walianza kwa kasi kubwa (Sijui waliambiwa nini na kocha Dunga) na walipata goli la kwanza sekunde 45 tu baada ya kipindi cha pili kuanza lililofungwa na Luis Fabiano. Brazil walipata mori baada ya goli hilo na walizidi kushambulia baada ya kufanya mabadiliko ya kuwatoa A. Santos na Ramires na kuwaingiza Elano na Daniel Alves . Luis Fabiano alisawazisha kwa Brazil kwenye dakika ya 74. Kwenye dakika ya 83 Brazil walikata mzizi wa fitina, kona ilipigwa na Lucio akafunga goli la tatu na la ushindi.

Hii ni mara ya tatu Brazil kuchukua kombe la Confederation (1997, 2005 na 2009)

No comments: