Thursday, June 18, 2009

Mapenzi mazuri yaleta

ufanisi kazini






Kuna mahusiano kati ya ufanisi wako kazini na maisha ya kimaingiliano kimapenzi (Sex life). Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya tafiti iliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Gothenborg nchini Sweden

Tafiti hiyo inabainisha mahusiano mema ya kimapenzi baina ya wawili wapendanao na maingiliano ya kimapenzi yenye furaha kwa wapendanao hupelekea kupungua kwa msongo na hata hatari za kuwa na afya mbaya kwa mtu aliye kazini.

Kinyume chake kwa maana ya mahusiano na maingiliano ya kimapenzi yasiyoleta furaha hupelekea hali ya msononeko na hata matatizo ya mara kwa mara ya kukosa usingizi.

Tafiti hiyo inaonyesha pia, kuwa kuridhika kimapenzi hutofautiana baina ya mwanamke na mwanamme. Kwa wanaume wengi, tendo la ndoa hupelekea kuridhika kimapenzi. Kwa mwanamke, kuridhika kimapenzi inaendana na mahusiano mengine ikiwamo kukumbatiana na kuwasiliana.

No comments: