Monday, June 08, 2009

Mwanafunzi Chuo Kikuu

Dar es Salaam auawa

kwa wivu wa mapenzi




Mwananchi

MWANAFUNZI mmoja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (Duce), ameuawa kwa kuchomwa kisu mara nne na mwanafunzi mwenzake kwa madai ya wivu wa mapenzi.

Inadaiwa mwanafunzi huyo, Bertha Mwarabu, 23, wa mwaka wa pili, alitofautiana na mpenzi wake, Masamba Musiba, 27, katika masuala ya mapenzi wakiwa katika hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu iliyopo Mabibo.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 2:30 usiku kwenye varanda ya Jengo 'C' la hosteli hiyo linalotumiwa na wanafunzi wa kike na kiume, lakini mauaji yalifanyika katika upande wa wanawake….bofya na endelea>>>>>

 

Mtanzania

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Elimu, Bertha Mwarabu, (23), ameuawa kwa kuchomwa na kisu na mwanafunzi mwenzake katika tukio linaloelezwa kuwa limesababishwa na wivu wa kimapenzi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Karunguyeye, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alieleza kuwa yalitokea juzi saa 4 usiku…bofya na endelea>>>>>

 

Habari Leo

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bertha Mwarabu, amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu tumboni na mwanafunzi mwenzake katika kinachodaiwa kuwa ni ugomvi wa mapenzi. Bertha anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 23 na 24, alikutwa na mauti juzi usiku katika Hosteli za Chuo Kikuu Mabibo, baada ya kushambuliwa kwa visu kadhaa mwilini hasa tumboni na mwanafunzi mwenzake wa DUCE, Masamba Musiba anayedaiwa alikuwa ni mpenzi wake wa muda mrefu….bofya na endelea>>>>> 

No comments: