Thursday, June 18, 2009

Obama akiua nzi!!!







Rais Barack Obama alikuwa akifanya mahojiano na televisheni ya CNBC wakati nzi aliyekuwepo kwenye ukumbi huo alipoanza kumghasighasi Obama.

Obama alijaribu kumfukuza nzi huyo kwa mikono yake lakini wapi nzi huyo king'ang'anizi alikuwa anarudi tu.

"Hey, hebu toka hapa " Obama alimwambia nzi huyo na kumfukuza tena kwa mikono yake.

Nzi huyo aliporudi tena Obama alimvizia kwa kumwekea mkono wake wa kushoto atue hapo na alipotua tu alimmaliza kwa pigo moja tu la mkono wa kulia.

"Safi sana" alisema mtangazaji aliyekuwa akimfanyia Obama mahojiano wakati Obama akimwonyesha mpiga picha nzi huyo kwenye zulia.

Chini ni video mbili za tukio hilo, ya kwanza inaoonyesha jinsi tukio hilo lilivyotokea wakati ya pili inaonyesha jamaa walivyotia chumvi kuhusiana na tukio hilo.


No comments: