Saturday, July 11, 2009

Tahadhari :

Wizi wa kadi za benki


Wizi wa kadi za benki au mikopo umeenea sana dunia nzima na unawaliza watu kila kukicha duniani kote. Benki za nchi nyingi hazina kiwango cha juu cha ulinzi wa uhalifu huu, sasa ni kwako wewe mtumiaji wa kadi hizi za kutolea pesa kujikinga kadri ya uwezo wako kabla hujalizwa na wajanja.

Utaalamu wa hali ya juu hutumika ili kukamilisha zoezi hili haramu, lakini pengine ni utovu wa nidhamu na upungufu wa uadilifu makazini au kutokuwa na elimu ya kujikinga kwa watumiaji kadi na mtandao wa internet huchangia. Huenda rushwa inachukua mkondo wake, na pengine baadhi ya wafanyazi wachache sana wasio waadilifu hutoa taarifa muhimu sana kwa wahalifu ili swala hili liweze kufanikiwakirahisi.

Zipo njia mbali mbali nyingi mno za kuweza kuwaibia watu kirahisi pesa zao aidha kwa kutoa pesa kwenye akaunti husika au kufanya manunuzi bila indini ya mmiliki wa kadi hiyo. Hili huwezakana kwa kutumia kivuli cha kadi zako za benki au tarakimu maalumu za kadi hiyo, mfano; kuna utaalamu wa kunakili taarifa muhimu za kadi kama vile namba ya akauti kwa kutumia vifaa mbali mbali (cloning devices). Njia nyingine ni kutumia ujanja wa kunakili pembeni au kukariri tarakimu za kadi ya mlengwa na kuzitumia kwa manunuzi yasiyo halali pasi naye kujua au kuiiba kabisa hiyo kadi na kufanya ujanja wa kutambua namba ya siri ya mmiliki wa kadi hiyo.

Fanya yafuatayo kujikinga.


1. Hakikisha Unajali kadi yako ya benki kama unavyozijali pesa zako (huwezi kuziacha hovyo hovyo bila uangalifu)

2. Hakikisha Humwambii mtu namba ya kadi yako hata kama unamuamini (hii haimaanishi kwamba huwaamini na huwajali, la hasha ni njia tu ya kujikinga kwani hujui nani muhalifu na nani si muhalifu, huenda Mke au mumeo nk.. akakuliza)

3. Weka sahihi kwa kalamu yenye wino wa kudumu au utakaokaa muda mrefu katika kila kadi yako ya benki kwenye ufito mwembamba nyuma ya kadi

4. Haribu kadi zako za zamani zinapomaliza muda wake.

5. Hesabu vizuri manunuzi yako kabla ya kutia sahihi risiti ya manunuzi, hakikisha hakuna nafasi zilizo wazi au manunuzi usiyoyafahamu.

6. Kabla ya kuharibu au kutupa Bank Statement zako, hakikisha unazichana chana katika vipande vidogo vidogo sana.

7. Itaarifu benki au kampuni iliyokupa kadi kama unasafiri nje ya nchi

8. Itaarifu benki au kampuni iliyokupa kadi mabadiliko yeyote ya anuani punde tu unapobadili makazi au sehem unayopokea barua zako.

9. Itaarifu benki au kampuni iliyokupa kadi haraka iwezekanavyo utakapoipoteza kadi yako

10. Usitoe namba au taarifa za kadi yako kwa njia ya simu ila tu unapokuwa na uhakika unayeongea naye anahusika na atakuhifadhi na uhalifu wa kadi za benki.

11. Hakikisha unapotumia kadi zako kwenye mtandao wa internet, unaiamini tovuti husika, na umewasha Kopi Halisi na halali ya Antivirus. Jiepushe na kopi feki za antivirus na usitumie kompyuta isiyo yako kufanya manunuzi au kuingiza namba za kadi yako kwenye mtandao wowote (unapofanya kinyume na hivi elewa hatari yake na jikinge). Update Antivirus yako automatiki. Hakikisha kila wakati inafanya kazi.

No comments: