Mwizi mkubwa wa
mtandaoni ambaye
hajawahi kutokea
Kijana mmoja Mmarekani (hacker) ameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya namba za siri za kadi za benki milioni 170.
Albert Gonzalez (miaka 28) akishirikiana na washkaji wake wawili wa Kirusi wamefanikiwa kuingia kwenye ”data network” za maduka makubwa duniani, mahoteli na makampuni ya kadi za benki.
Mwanzoni, Gonzalez alikuwa akiwasaidia US Secret Service, kuwasaka waibaji wa mtandaoni, lakini jamaa wa Secret Service walianza kumtilia mashaka yeye mwenyewe, ndipo walipomwekea mtego na kumnasa na kugundua kuwa ni mwizi wa mtandaoni ambaye hajapata kutokea hadi sasa.
Akipatikana na makosa, ana heka heka ya kufungwa maisha.
No comments:
Post a Comment