Sunday, August 16, 2009

Usain Bolt avunja rekodi

yake ya dunia






Mjamaika Usain Bolt amevunja rekodi ya dunia ya mita 100 kwenye uwanja wa Olimpiki mjini Berlin, kwenye mashindano ya riadha ya dunia. Ameweka rekodi mpya ya dunia ya sekunde 9.58 na kuvunja rekodi aliyoiweka siku 365 zilizopita kwenye michezo ya Olimpiki mjini Beijing. Mtetezi wa rekodi, Mmarekani Tyson Gay alikuwa wa pili kwa sekunde 9.71, wakati Mjamaika mwingine, Asafa Powell alikuwa wa tatu kwa sekunde 9.84. Kwa rekodi hii, Bolt amevunja kilimilimi cha kuwa nani mkimbiaji bingwa duniani.


No comments: