Mama yao alitaka kuwakata
vichwa: Kisa na mkasa;
eti ni wachawi
Watoto hawa wawili; Jane (kushoto) na Mary (kulia) wameponea chupuchupu kuuawa na familia zao nchini Naijeria. Sababu kubwa kasisi wa kanisa la mahali wanapoishi aliwashutumu kuwa ni wachawi. Mama yao kwanza alimlipa kasisi huyo ili awaondoe mizimu, iliposhindikana; mama akachukua sheria mkononi kwa kutaka kumkata kichwa mtoto wake ili amwondoe uchawi. Idadi ya watoto wanaoshutumiwa kuwa ni wachawi nchini Naijeria ni 15000 (kumi na tano elfu) kwenye jimbo la Akwa Abom na Eket kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Kati ya hao; 1000 wameuawa kwa kudhaniwa ni wachawi.
Cha kusikitisha ni kuwa makanisa ya madhehebu ya ajabu ajabu ndiyo yanayohusika na tuhuma hizi. Mengi ya madhehebu haya yanachanganya mila na desturi na dini kwenye mafundisho yao.
No comments:
Post a Comment