Friday, October 23, 2009

Mtoto wa miaka miwili

afariki kwa mafua ya nguruwe

Waziri wa afya:

Wananchi wote wachanjwe!



Waziri wa afya, Anne-Grete Stroem Erichsen.


Mtoto mmoja wa miaka miwili amefariki kwa mafua ya nguruwe na kuwa mtu wa kumi kufariki kwa mafua ya nguruwe hapa Norway. Mtoto huyo amefariki kwenye hospitali ya Sorlandet. Amesema daktari mwandamizi Bjoern Iversen wa kitengo cha mamlaka ya afya (Folkehelseinstituttet).

Wakati huo huo kwenye kikao cha dharura cha hali ya hatari ya mafua ya nguruwe; waziri wa afya, Anne-Grete Stroem Erichsen anawaomba wananchi wote wa Norway kukubali na kwenda kuchanjwa Pandemrix (chanjo ya mafua ya nguruwe).

Wananchi wengi wamekuwa na wasiwasi na athari za chanjo hiyo; kwani haijafanyiwa majaribio ya kina. Wataalamu wa afya wanawaondoa wananchi hofu kwa kusema kuwa chanjo hiyo iko salama na haina madhara.

Bofya na soma zaidi kuhusu Pandemrix

Soma pia: http://www.legemiddelverket.no/templates/InterPage____80892.aspx (Kwa Kinorwejiani)


No comments: