Vipipi vimekuwa kama upupu
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Habari za leo kijana mwenzangu? U mzima au wazimu? Maana tunavyozimwa katika mambo yetu wazimu hauwezi kukaa mbali sana. Kweli kabisa mpenzi wangu. Ninapoangalia luninga siku mojamoja na kuona jinsi maendeleo ya nchi nyingine yanavyoletwa na vijana, najiuliza kwa nini hapa hatupati kitu zaidi ya kutupiwa vijisenti vinavyoitwa mabilioni.
No comments:
Post a Comment