Friday, October 16, 2009

Wanatafuta kutafuna kidogo na wao, kisha?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

Mpenzi Frank,

Lo! Wiki nyingine imepotea hivihivi tu mpenzi huku nikikuwazia bila kukuona. Vipi mambo zako huko mwekezaji wangu? Biashara imeanza kufufuka kidogo baada ya zahama kuhama na kuhamia kwetu? Hata hivyo nawashangaa watu wengine hapa. Hawajui zahama wala mtoto wake zahama. Hebu fanya hesabu. Matumizi ya simu kwake si chini ya shilingi elfu tatu kwa siku. Haya elfu tisini tu kwa ajili ya simu! Halafu, kwenye baa hakosekani kila siku, angalau bia mbili Si elfu tisini tena. Hapa hajalipa kodi ya pango, wala nauli za kila siku, licha ya chakula kwa ajili yake na familia yake. Na jamaa mwenyewe wala hana kazi inayoeleweka.

…..Bofya na endelea>>>>>


No comments: