Wednesday, November 18, 2009

Awaita Waafrika:

Nusu nyani!!!!!



Roger Madsen picha ya kulia.


Naibu kiongozi wa Progressive Party, tawi la Moss, Bw. Roger Madsen amewaita Waafrika nusu nyani, kufuatilia ziara ya Mfalme Mtarajiwa wa Norway (Crown Prince) Haakon aliyoifanya Botswana wikiendi hii iliyopita. Madsen amesema Afrika kunakaa nusu nyani na itawachukua vizazi 2 au 3 kuanzia sasa kuwa wastaarabu.

Madsen alimlaumu Haakon kutembelea Afrika na alisema kuwa angeenda nchi za Asia badala yake.

Bofya uone na usome (ukom kwa Kinorwejiani): Mtandao jamii Facebook wa Mfalme Mtarajiwa Haaon

Chanzo cha habari: Moss Avis

2 comments:

Anonymous said...

Huyu jamaa namna gani? Anakaa karne ipi? Progressive Party wamfukuze...

Anonymous said...

Baadhi ya viongozi na baadhi ya wanachama wa Progressive Party ni makaburu; wabaguzi wa rangi wa kutupwa!