Monday, November 16, 2009

Faini au kifungo kwa ndoa batili


Sheria mpya ya wageni hapa Norway itaanza kutumika kuanzia Januari Mosi. Moja ya mabadiliko makubwa ya sheria hiyo, inahusu ndoa kati ya Mnorwejiani na mtu mwenye asili ya kigeni. Vitengo vinavyohusika, idara ya uhamiaji au polisi, vikitilia mashaka ndoa ya namna hii, basi bibi na bwana harusi wanaweza kupigwa faini kubwa au kifungo cha miaka mitatu ama vyote viwili. Na mwenye asili ya kigeni kufukuzwa nchini.


No comments: