Wednesday, November 11, 2009

FUNDI CHEREHANI NA BIBLIA!


Fundi cherehani mmoja alikuwa hoi baada ya kuingia mteja wake mmoja mrembo sana! Mrembo huyo alikuja kupima kitambaa ili ashonewe gauni; Ile kumtazama jinsi alivyoumbika, fundi uchu ukamshika.

Basi wakati anampima akawa anaitumia nafsi hiyo kumshikashika mara kifuani, mara hips huku akijichelewesha kumpima taratibu. Yule mrembo kuona vile hakuvumilia, ndipo akamwambia Fundi; We, fundi kumbuka Mathayo 7:7, kusikia hivyo fundi akaogopa kwa kudhani amekutana na mlokole ikabidi kwa hofu asitishe mchezo wake.

Basi alipomaliza kumpima, yule mrembo aliondoka. Fundi haraka sana akachukua Biblia na kuanza kusoma Mathayo 7:7. Lahaula alikutana na maneno haya; “Ombeni nanyi mtapewa! Pale pale aliitupa Biblia mezani na kutimua mbio kumfuata yule mrembo.


No comments: