
Ghafla vijana tumeanza
kuonekana lulu!
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Nilijua tu utacheki na kucheka ung’eng’e wangu. Potelea mbali, hata Waziri Mkuu wa Japan hawezi kuongea Kiingereza! Lakini kwenda kuwasomea marafiki zako mpenzi ... vibaya hivyo jamani! Bila shaka walimcheka sana mchumba wako hata kama na wao hawawezi pia. Sijui lini tutaacha kutumia lugha ya wengine kama kigezo cha maendeleo. Lakini pamoja na vicheko vyako, nakumiss, nakumiss, nakumiss sana. Natamani kuimba ... usende mbali nami ... mimi nakupenda, usondoke mbali na mi ... lakini ukweli ni kwamba uko mbali hivyo bora niimbie sogea karibu na mii ... mimi nikupendee ... njoo karibu namii ... nikukumbatie ....
No comments:
Post a Comment