Wednesday, November 25, 2009

Norway


Mtu wa 25 afariki kwa mafua ya nguruwe


Leo hii mtu mmoja mwenye miaka 25 amefariki kwa mafua ya nguruwe hapa Norway. Mtu huyo amefariki kwenye mkoa wa Oppland na amekuwa wa 25 kufariki kwa mafua ya nguruwe nchini. Kufariki kwa mtu huyo kumethibitishwa na mganga mkuu kwenye idara ya afya (Folkehelseinstituttet) Dk. Bjørn Iversen. Watu 60 wamelazwa kwenye hospitali mbali mbali na 13 kati yao wako mahututi.

Karibu watu wote ambao wako kwenye makundi ya watu wasio na afya nzuri, wameshachanjwa dawa za kuzuia ugonjwa huu, na wiki hii wanafunzi kwenye shule za msingi hapa Oslo, wameanza kuchanjwa.

Kumekuwa na watu wanaotilia mashaka dawa za kuzuia mafua zilizokubaliwa kutumika hapa Norway (Pendemrix). Wengi ya watu wa kundi hili wamefikia hatua ya kukataa kuchanjwa kwa kuhofia athari na madhara ya muda mrefu ya Pendemrix.

Kwa maelezo zaidi bofya na soma viungo hapo chini

http://www.helsedirektoratet.no/vp/multimedia/archive/00269/ENGELSK-201109_269459a.pdf

http://www.helsedirektoratet.no/vp/multimedia/archive/00248/Engelsk_-_Kort_publ_248269a.pdf

http://www.pandemi.no/pandemi/information_regarding_the_new_influenza__swine_flu__392754


No comments: