Tuesday, November 17, 2009

Raia 19 wa Pakistan wanaswa

kwa kuingia kinyemela




Kiyao Hoza

Raia wa Pakistan 18 walioingia nchini kinyemela, wanashikiliwa na Polisi baada ya kunaswa wakiwa njiani kuelekea Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova, amesema wahamiaji hao haramu walidakwa pale Mtoni Mtongani, jirani na daraja la mto Kizinga.

Akasema kabla ya kukamatwa, askari walikuwa kwenye doria ndipo walipoyastukia magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser.

Ameyataja mgari hayo kuwa ni yenye namba za usajili T307AAN na T454ADS.

Kamanda Kova amesema kwa mujibu wa maelezo ya wahamiaji hao walikuwa njiani kuelekea Mtwara ingawa hawakuwa na vibali vyovyote vinavyowaruhusu kuingia nchini.

Akasema watuhumiwa hao wanadaiwa kuingia nchini mmoja mmoja na kujikusanya kabla ya kupanga safari yao hiyo.

Watuhumiwa hao wametambulika kuwa ni Maliesi Muhamad Ally, 19, Chaundhry Huran ,22, Ageel Ashraju, 20 na Ahsan Ally, 20.

Wengine ni Muhsin Raza ,18, Abdulaziz Aziz, 35, Sajda Igbal, 29, Muhsin Intiazi, 24, Asij Iqbal,19, Assad Butt, 28 na Farkhar Abbas,14.

Pia, wengine ni Hurag Zeb ,25, Muhamad Riziwan ,28, Ahsani Khan, 27, Zakiri Khan ,25, Jaza Knarid ,20, Muhammad Ajzal, 27 na Mohamed Warbaicha, 35.

Ameongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini ukweli zaidi kuhusu watu hao kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa.

ALASIRI

No comments: