Thursday, November 19, 2009

Semenya hatanyang´anywa

Medali ya dhahabu




Shirikisho la michezo ya riadha duniani, IAAF, limeamua kuwa Caster Semenya, abaki na medali ya dhahabu ya mbio za mita 800, aliyoipata kwenye fainali za michezo ya riadha ya dunia iliyofanyika Berlin, Agosti mwaka huu.

Makubaliano kati ya IAAF na wakili wa Semenya yamefikiwa leo baada ya matokeo ya vipimo vya jinsia ya Semenya kujulikana leo. Jinsia ya Semenya inabaki kuwa siri kwenye makubaliano hayo.

Chanzo cha habari: Reuters

No comments: