Thursday, November 05, 2009

Tovuti 5000 za Kinorwejiani

zashambuliwa na mahaka (hackers)


Tovuti karibu 5000 za Kinorwejiani zimeshambuliwa na mahaka (hackers) kutoka nje ya Norway. Mahaka wengi wamekuwa wakiweka program za kijasusi kwa minajili ya kuiba koda (codes) na habari binafsi za walengwa. Hayo yamesemwa na Preben Nykoekken, mshauri mwandamizi wa masuala ya usalama wa Teknohama wa kampuni iitwayo Watchcom.

Wenye kompyuta majumbani wanashauriwa ku´upgrade program za kulinda usalama. Microsoft wana program iitwayo Windows Security Essentials ambayo mtu anaweza kuifyonza bure bileshi. Kuna zingine za bure kama Avira AntiVir Personal, Avast Antivirus Home Edition,AVG Anti-Virus Free Edition 8.5. Zingine zinapatikana kwenye www.download.com

No comments: