Wabongo hivi mpaka lini?
Kila kitu tuongozwe?
Haya wakuu na mimi sikukosekana pale Neshno jipya kwenye mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, haya ndiyo niliyojionea.
Kwa kweli Watanzania nashindwa kuelewa sijui tukoje. Manake kwenye vile vyoo vya Neshno Stadium yale masinki ya kunawia ndio yaligeuzwa sehemu ya kukojolea!!!
Hii ni aibu sijui ni ustaarabu gani? Watu wengine sijui wakoje, yaani choo kipo na kawekewa kila kitu, lakini wanaacha kujisaidia sehemu husika, wanaenda kujisaidia sehemu ya kunawia kama inavyoonekana kwenye picha.
Watanzania ustaarabu uko wapi?
Cha pili, kingine nilishangaa sana yaani muda wa half time, kituko kingine:
Wanaume mibaba mizima inaingia kujisaidia kwenye vyoo vya kike wakati vyoo vya wanaume vipo!!!
Yaani ilikuwa tafrani mpaka akawekwa polisi kwenye mlango wa choo cha wanawake ili jamaa wasiingie…..
Wabongo yaani kila kitu mpaka tuongozwe.
La mwisho msihofu wana YANGA ushindi wa kagoli kamoja. Walibahatisha tu marudiano tutashinda tu
Mdau DX Werre
No comments:
Post a Comment