Krismasi nyeupe kama theluji!
Ni miaka kadhaa hapa Oslo, tumesherehekea Krimasi nyeupe kama theluji. Mwaka juzi na mwaka jana, theluji ilianguka baada ya Desemba 24. Mwaka huu majira ya theluji yameanza mapema na theluji imekuwa ikianguka kwa siku kadhaa sasa. Picha hizo hapo chini zimechukuliwa leo mchana, zinaonyesha jinsi theluji ilivyotanda hapa Oslo. Halibaridi imefikia hadi kati ya 7 hadi 16 chini ya nyuzi za baridi.
Halibaridi = minus temperature
Theluji = snow
Barafu = ice
Mhariri ametoa hii leo kwa sababu wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanashindwa kutofautisha matumizi ya neno ”theluji” na ”barafu”. Utasikia mtu anasema leo imeanguka barafu nyingi.
Wakati ikianguka inaitwa ”theluji”. Itakapoganda ardhini na kuwa kama kioo, ndipo inageuka na kuitwa ”barafu”!!!
Iliyopo kwenye picha hizo hapo juu ni ”theluji” na siyo ”barafu!”na
2 comments:
Ndugu mhariri..
Swadakta!
Wapashe! Bora hata hao wasiotofautisha barafu na theluji. Kuna wengine ndio wanachemsha vibaya mno. Utawasikia:
Leo "snow" imeanguka.
Huwa nashikwa na kichefuchefu!
Post a Comment