Mwanamke wa kwanza
kukatiza Antarktis
Cecilie Skog. Picha na Åse Liserud/SCANPIX.
Mwanadada wa Kinorwejiani, Cecilie Skog (35), amekuwa mwanamke wa kwanza kukatiza ncha ya kusini ya dunia, Antarktis. Cecilie alikuwa na Mwamerika, Ryan Waters (36). Hii ni historia kwani ni mara ya kwanza kwa binadamu kukatiza ncha ya kusini kwa kutembea kwa kutumia ”ski” bila ya msaada wa aina yoyote.
Walihitimisha safari yao jana Alhamisi Januari 21 kwenye ncha ya barafu iitwayo Ross, Antarktis. Safari yao ilianzia kwenye kisiwa cha Berkner, Novemba 3, mwaka jana. Walifika kwenye ncha ya kusini kwenye mkesha wa kuamkia 2010 baada ya kutembea kwa siku 49. Baada ya hapo wakaanza safari ya kukatiza hilo kontinenti la barafu. Safari hiyo imewachukua kilomita 1800 kwenye nyuzi za baridi -60oC hadi -70oC.
Cecilie akizungumza kwenye simu ya satelaiti amesema anasikia njaa na ana amepungua na ana kilo 45.

No comments:
Post a Comment