Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Vipi hali yako mpenzi. Mimi ni mzima huku nikiwa na wazimu wa kukumbatia mto nikifikiria ni wewe. Jamani! Bado nang’aa kwa raha ya kukuona wiki juzi lakini sasa najiuliza tutaonana lini tena. Wewe ni dawa ya kulevya Bwana. Nikishaonja siwezi kuishi bila kuonja tena. Lakini usiwe na wasiwasi mpenzi. Siwezi hata kueleza jinsi nilivyopata nguvu mpya kwa kukuona tena. Dawa ya kulevya nakuambia.

No comments:
Post a Comment