Serikali ya mseto
Kwanza natowa shukrani kwa viongozi wa vyama viwili CCM & CUF kukubaliana kukaa upya kuzungumzia masuala ya matatizo ya uchaguzi wa ZANZIBAR. hapa wameonesha uzalendo halisi kwa faida ya nchi yetu , wahenga wamesema (in politics there is no enemy) lazima wanasiana baada ya uhasama watakaa juu ya meza na kupeana mikono.
MADA YA KUJADILIWA
(serikali ya mseto)
Hivi katiba ya nchi inaruhusu kuwa na serikali ya mseto ?? Au katika nchi yetu rais anaweza kuamua kuunda serikali ya mseto??
Hapa ninachoshaanga zaidi hivi vyama vya upinzani vingine ambavyo havikuwa hata kwenye uchaguzi wa ZANZIBAR na nyenginevyo vilikuwa ndani ya uchaguzi lakini hawakupata kura, lakini wanalilia kuwa kwanini hawawakilishwi kwenye vikao vya muafaka na wanahoji kwamba lazima na wao wawepo kwenye serikali ya ya mseto jee hii ni sahihi ??
Mimi nimeishi miaka 25 Norway na kwa muda huo serikali 5 zimeudwa za mseto na hata hii iliyokuwa madarakani ni ya mseto.
Hapa ninachojuwa kwamba serikali ya mseto huundwa baada ya kila mshirika kuleta kura zake alizoshinda na atapata ushirika wa kuunda serikali kutokana na wingi wa kura zake .kwa mfano nchi ina wizara 15 kwa maana hii chama (A)kimepata aslimia 40 chama( B) aslimia 15, chama (C) aslimia 10. kwenye serikali hiyo chama A kitachukua wizara muhimu kuliko vyama vingine japokuwa kwa idadi watagawana kutokana na wingi wa mavuno ya kura zao kwa kila chama.
Lakini hapa kila chama huingia kwenye uchaguzi kivyake ila vyama huwa na mahusiano tangu mwazo kuna mlingo wa kulia na mlingo wa kushoto kikawaida chama cha mlingo wa kulia hushirikiana na mlingo wa kulia. baada ya uchaguzi matokeo yakitokea kama hakuna chama kilichojinyakulia ushindi wa kuchukua serikali. Hapo mlingo mmoja hutafuta muafaka kwa mweziwe na kuunganisha matokeo ya kura zao ili waweze kuunda serikali ya mseto . Jee mfumo huu unaruhusu TANZANIA AU HUKO ZANZIBAR ????
Sasa hivi vyama vinavyosema navyo vinataka kuwepo kwenye muafaka wakati havina kura za huko ZANZIBAR vinakuwa havielewi siasa au vinataka malumbano tuu.
Ushauri wangu hivi vyama vingine vielewe kwamba ili kuingia kwenye mseto wajitahidi kupanda mchele au choroko mapema kwani uchaguzi ni miezi 11 ijayo kuanzia sasa na wakishindwa kuvuna mchele au choroko hata maji ya KILIMANJARO (kura chache) yatasonga mseto
MUNGU IBARIKI TANZANIA
SLIM
OSLO,
NORWAY.
OSLO,
NORWAY.

No comments:
Post a Comment