Saturday, January 30, 2010


Ufaransa kupiga marufuku Niqab
(mabaibui yanayoziba uso mzima)














Waziri Mkuu wa Ufaransa, Francois Fillon anaangalia uwezekano wa kutunga mswada wa sheria kuhusu Niqa (mabaibui yanayoziba uso mzima). Juzi Jumatatu wabunge wa Ufaransa wamekubali kuwa uvaaji wa vazi hilo ni udhalilishaji wa mwanamke na upigwe marufuku kwenye sehemu za umma kama vile mashuleni, kwenye sekta ya usafiri, makazini na kwenye sekta ya uhudumiaji. Wabunge hao wamependekeza wananchi wasikilizwe na watoe maoni yao kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa. Baada ya miezi sita ipitishwe sheria ya kupiga marufuku uvaaji wa vazi hilo.

No comments: