Hofu ya bomu Msasani
Wakazi wa Msasani Bonde la Mpunga eneo la Maandazi Road jijini Dar es Salaam, leo walikumbwa na hofu baada ya mtu asiyejulikana kutelekeza bomu kwenye kichochoro kimoja mtaani hapo. Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Bi. Rose Temu, alisema kijana mmoja alionekana mtaani hapo akitafuta mtu wa kumuuzia bomu hilo kama chuma chakavu lakini wanunuzi walionesha wasiwasi kuwa huenda ni bomu ndipo kijana huyo aliamua kulitelekeza mtaani hapo. Kufuatia tukio hilo kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kikosi maalum cha kutegua mabomu, kilifika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa ni bomu hatari na kulichukua na kuondoka nalo.
2 comments:
Kweli Tanzania tuna safari ndefu!
Angalia hao wanajeshi wa JWTZ. Hao ndio wa kikosi maalumu cha mabomu!!!
Wao wenyewe ni mabomu!!!
Hawana vifaa vya kutegua mabomu?!
halafu wameruhusu watu kuwazunguka kiasi hicho. Je, lingelipuka?
Nilitarajia kuona askari wa JWTZ akiwa full mziki namna hii:
http://www.goochlandgazette.com/midlothianexchange/images/uploads/MX_040909_bombsquar1A.jpg
Duh....lakini wapi!!!
Sijui lini tutajifunza?!
Post a Comment