Mada ya wiki hapa Norway:
Ruzuku kwa vyama vya wageni
Aftenposten, 23.02.2010
Kuanzia Jumanne wiki hii hapa Norway kumekuwa na gumzo kwenye magazeti, haswa gazeti kubwa la kila siku la Aftenposten kuhusu ya ruzuku na hela zinazotolewa na Manispaa na serikali kuu kwenye vyama vya kijamii vya watu wenye asili ya nje ya Norway.
Aftenposten, 23.02.2010
Wadau wanaopinga kutolewa kwa ruzuku kwa hivi vyama, wanadai kuwa lengo hasa la utoaji wa hizo hela limepotea kwani hela wanazopewa vyama vya wageni na shughuli zao wanazofanya, haziendani kabisa na lengo asili la ruzuku hizi. Badala ya kuwajumuisha wageni na wazawa kwa pamoja, matokeo yake ni kuwa wageni wengi wamekuwa wakijitenga kwa kutumia miamvuli ya vyama vyao na shughuli zao, ambazo nyingi ya hizi shughuli haziwajumuishi wazawa hata kidogo. Badala yake, wageni hujitenga badala ya kujijumuisha kwa pamoja na wazawa.
Aftenposten, 23.02.2010
Aftenposten limegundua kuwa vingi ya hivi vyama vinaendeshwa kwa kujuana, kindugu, kikabila, kitabaka na kadhalika.
Mfano uliotolewa iweje kuwe na zaidi ya vyama 54 vya watu wenye asili ya Somalia, kwanini pasiwe na chama kimoja kikuu chenye lengo la kuwaunganisha Wasomali wote, badala yake kuwe na vyama vingi vyenye lengo la kuzidi kuwatenganisha Wasomali na bado Manispaa na serikali inatoa hela kwa hivi vyama bila ya kufuatilia na kujua lengo haswa la hivi vyama na jinsi hela zinavyotumika.
* Wasomali wana vyama 54
* Wapakistani wana vyama 46
* Waturuki wana vyama 14
* Watamili wana vyama 13
Aftenposten, 24.02.2010
Au mfano mwingine, iweje kuwe na chama cha maskauti wa Kiislamu na bado kipewe ruzuku badala ya kuwa na chama cha maskauti kinachowajumuisha vijana wote, wakiwepo wa jinsia tofauti, dini tofauti na asili tofauti.
Aftenposten, 25.02.2010
Mfano mwingine ni baadhi ya hivi vyama kuandikishwa kwa jina la mtu mmoja, lakini bado huyo mtu ana wanachama wanaolipa ada za mwaka na huyu mtu anaweza kuomba pesa na bado akapewa, bila ya kufuatiliwa kwa undani zaidi ni nini hasa lengo la shughuli zake. Wengi wenye vyama vya namna hii ni watu wenye asili ya Pakistan. Si muda mrefu uliopita, iligundulika kuwa baadhi ya hawa hawa watu wamechukua mamilioni ya hizi ruzuku na kujijengea mahekalu huko Pakistan.
Vyama hivi, huandika miradi kama inavyotakiwa kwenye masharti ya maombi, lakini vikishapata hela, zinavyotumika hizo hela haijulikani.
Wadau wanaopinga ruzuku za namna hizi, wanaomba serikali za mitaa na serikali kuu zisitishe kwa muda utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya kigeni, pafanyike utafiti wa kina juu ya hizi ruzuku kabla ya kuondelea kutolewa. Wadau hawa wanadai kuwa kuna vyama vingi tu vinavyojiendesha bila kutegemea hizi ruzuku. Kama hivi vyama vinaweza kujiendesha bila ruzuku kwa nini nini hivyo vingine zisiweza kujiendesha bila kupewa ruzuku.
Tunasubiri usemi kutoka kwenye serikali za mitaa na serikali kuu juu ya hizi ruzuku. Huenda labda vyama vya upinzani vikajipatia pointi kwenye hili suala.
Yetu macho na masikio!
na mhariri wa blogu.
Tanbihi: Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo), kimekuwa kikijiendesha bila ruzuku toka kwenye Manispaa ya Oslo au serikali kuu kwa muda mrefu. Shughuli nyingi za CCW Oslo zimekuwa za kujitolea toka kwa baadhi ya Watanzania na jamaa zao waishio Oslo, Akershus na Norway kote.
Tanbihi: Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo), kimekuwa kikijiendesha bila ruzuku toka kwenye Manispaa ya Oslo au serikali kuu kwa muda mrefu. Shughuli nyingi za CCW Oslo zimekuwa za kujitolea toka kwa baadhi ya Watanzania na jamaa zao waishio Oslo, Akershus na Norway kote.
4 comments:
MHARIRI WA BLOGU, ASANTE SANA KWA MAKALA HII...
UKIPATA MUDA FANYA HIVI KILA WIKI.
MMSOMAJI WA KILA SIKU WA BLOGU HIII...
Namwunga mkono Dotto.
Ukipata nafasi compile habari kama ulizofanya hizi. Tunajua hapa majukumu na mihangaiko mingi lakini jitahidi.
mi nipo bongo lakini kila siku lazima nifungue blog hii zaidi ya mara moja japo huku gharama za internet cafe ziko juu. jambo lingine hebu tupatie mara nyingine makala kuhusu hawa ndugu zetu walioko huko katika mihangaiko almaarufu WABEBA BOX tunapenda sana kujua mambo yao tumekuwa tukisikia tu wabebabox wa uk watujasikia wabebabox wa norway please.
Wanorwejiani wapo wachacha sana kiasi kama milioni tano tu. Wageni tuko wachache ukilinganisha na nchi zingine za Skandinavia au Uingereza.
Nchi yao iko "organized" kiasi ambacho chochote mtu anachofanya kinajulikana.
Ukipata kibali cha kuishi na kufanya kazi, basi unapewa namba kumi na moja za kitaifa "social security number". Hapo tayari unakuwa kwenye "database" ya taifa. Chochote utakachotaka kufanya lazima hizo namba zako kumi na moja uzitoe.
Ukienda kwa daktari, ukienda banki, ukienda kunuanua SIM card ili upata namba ya simu lazima utoe. Karibu kila kona na nyanja ya maisha ya kila siku hizo namba kumi na moja zinahitajika. Na kila kazi utakayofanya au shughuli utakayofanya ya kukupatia pesa, lazima utajulikana.
Na ukujulikana, jamaa wa kodi watakukaba koo, uwamegee chao.
Hakuna wamachinga wala wabebabox kama mabavyo wako Uingereza na kwingine.
Hii haina maana ya kuwa hakuna wezi, vibaka na mambo ya namna hii la hasha, ila ni kuwa kwa jnsi nchi yao ilivyo "organized", mihangaiko kama ya Uingereza au nchi zingine ni vigumu kweli.
Post a Comment