Tuesday, February 16, 2010

Bagamoyo, Tanzania

MALI za aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ambaye alivuliwa wadhifa huo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hivi karibuni kwa tuhuma za ufisadi wa mali za umma, Michael Karoli Wage, zinachunguzwa huku baadhi ya watu wakipigwa na mshangao kwa baadhi ya vitu anavyodaiwa kuvimiliki, UWAZI limebaini

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, Bagamoyo na Morogoro umebaini kuwa vyombo mbalimbali vya dola vinamchunguza Wage, ambaye pia hujulikana kama Kigogo wa Mtangazaji Jerry Murro aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa, kutokana na kuwepo madai mbalimbali juu ya umiliki wake wa mali zilizosheheni utajiri uliopindukia.

Anahusishwa na kumiliki shilingi bilioni mbili, ghorofa 6, Benz la milioni 200, hoteli na mali lukuki.

No comments: