Waislamu waandamana
Waislamu wapatao zaidi ya 3000 waliandamana leo alasiri baada ya sala ya Ijumaa.
Waandamanaji kadhaa walifanya sala ya alasiri kwenye mtaa wa Karl Johan nje ya kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Oslo.
Baada ya sala na mawaidha kadhaa, waandamanaji walitoka na kuelekea Stesheni Kuu Oslo, kupitia Karl Johan. Baada ya hapo, wakaelekea kwenye ofisi za gazeti la Dagbladet, lakini hawakufanikiwa kufika karibu na ofisi hizo, kwani kulikuwa na utitiri wa polisi waliokuwa wakilinda ofisi hizo.
No comments:
Post a Comment