Thursday, February 18, 2010

Oslo & Ski, Norway

Maji safi kuanzia kesho!


Maji ya kunywa kwenye Manispaa ya Oslo na Ski yatakuwa safi kuanzia kesho Ijumaa 19 Februari 2010. Toka juzi Jumanne, wakazi wa Manispaa hizi mbili walishauriwa kuchemsha maji kabla ya kuyanywa baada ya kugundulika uchafu kwenye maji ya kunywa. Baada ya uchunguzi wa kina, hakujagundulika bakteria kwenye maji ya kunywa kama ambavyo ilihofiwa mwanzoni.

Chanzo: NRK 

No comments: