Paka anayetabiri kifo!
Huyu paka anaitwa Oscar na amekuwa akiishi na kufanya kazi na Dk. David Dosa kwa miaka miwili kwenye makazi ya wazee Rhode Island, Marekani. Mara zote Oscar akienda kwa mzee na kukaa na kucheza naye, basi mzee huyo hufariki. Hiyo imetokea mara 50.
Dk. Dosa amesema kuwa paka huyo ananusa kifo kabla hakijatokea. Dk. Dosa ameandika makala ndogo kuhusu paka huyo kwenye jarida ”The New England Journal of Medicine.”

No comments:
Post a Comment