Monday, February 15, 2010

SINEMA MPYA YA KITANZANIA
KUTOKA UINGEREZA MWEZI UJAO


Na Freddy Macha, London


Sinema mpya, Lovely Gamble, katika Kiswahili na Kiingereza, inatazamiwa kufanyiwa sherehe rasmi kabla ya kuonyeshwa na kuuzwa ulimwenguni, mwezi ujao.

Watengezaji wa sinema hiyo, Frank Eyembe na Baraka Baraka, ambao ni Watanzania na wakazi Uingereza, wamesema mchezo una waigizaji wa Kiingereza na Kibongo akiwemo mwanatamthiliya wetu maarufu, Steve Kanumba na ina azma ya kufungua njia mpya ya utengenezaji picha kwa Watanzania.

Walifafanua: “Miaka ya karibuni tumeona sinema zikitolewa haraka haraka, kwa mwezi mmoja, kiholela na kuuzwa mitaani. Sinema hizi huwa zinawafaidi wafanyabiashara wanaowapa presha watengenezaji wanao lipua lipua tu. Utengenezaji sinema si suala la kulipua. Ila msanii akiambiwa atalipwa shilingi hamsini milioni anaona nyingi, kumbe mfanya biashara anabaki na haki miliki. Hatuwezi kuendelea mbele kama sinema zetu zitafuata masharti na matakwa ya hawa wafanya biashara na wamachinga.”

Kampuni ya Urban Pulse yenye makao mji wa Reading inawahusisha pia vijana na wananchi wa mataifa mbalimbali na pia wenyeji wa hapa Uingereza.

Karibuni kumekuwa na msisimko mkubwa wa sinema za Kibongo nyingi zinazotengenezwa vibaya jambo ambalo limewafanya Watanzania tusipende filamu zetu wenyewe na kukimbilia za wageni mathalan Wanaijeria.

Shirikisho jipya lililoundwa miezi michache kurekebisha hali ya sinema nchini, Tanzania Film Federation (TFF) limeweka vipengelee kadhaa vya kusaidia tatizo na kati yake ni kupanga haki miliki na kuzipanga sinema katika umri takikana (certification) kusaidia watengenezaji na wasambazaji kuzingatia maadili wanapoonyesha mahusiano ya kijinsia na mapenzi.

Tazama kipande:

No comments: