Saturday, February 06, 2010

Uturuki: Azikwa mzima mzima huku amesimama:Kisa na mkasa: amezungumza na wavulana

Msichana mmoja wa Kituruki mwenye umri wa miaka 16, Medine Memi ameuawa na baba na babu yake kama adhabu ya kuzungumza na wavulana.

Alifukuliwa na kukutwa amesimama na baada ya kupimwa akakutwa amejaa mchanga tumboni kitu ambacho kinaashiria kuwa alifukiwa mzima mzima akiwa hai. Msichana huyo alikuwa ametafutwa siku 40 kabla ya kujulikana nini kilichomsibu.

Mama wa binti huyo marehemu; Immihan amesema kuwa, Medine amewahi kukimbilia Polisi mara tatu, na mara zote hizo amekuwa akirudishwa nyumbani. Mauaji ya wasichana kwa sababu ya kushukiwa kuwa na marafiki wa kiume ni ya kawaida kwenye baadhi ya sehemu za Uturuki.

Mauaji hayo yametokea kwenye kijiji cha Kahta, Kusini Mashariki ya Uturuki.

No comments: