Monday, March 15, 2010

Askari Aliyekataa Rushwa Kiwanja
Cha Ndege Cha Mwalimu Nyerere
Jijini Dar Es Salaam Huyu Hapa



Askari Aliyekataa Rushwa Kiwanja Cha Ndege Cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar Es Salaam Huyu Hapa.



Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema akimkabidhi askari namba E. 7235 PC John Anthony Mwesongo wa kituo cha polisi cha Polisi Kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere hundi yake ya shilingi Milioni Nnne katika ukumbi wa maofisa wa polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Askari namba E. 7235 PC John Anthony Mwesongo wa kituo cha polisi cha Polisi Kiwa cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni mtunza vielelezo wa kituo hicho, akionyesha hundi ya T. Sh. 4,000,000 motisha baada ya kukataa rushwa ya dola za kimarekani 3,000 na watu waliokamatwa na madawa ya kulevya waliomtaka abadilishe vielelezo hivyo. Hundi hiyo alikabidhiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP),Saidi Mwema Jana katika ukumbi wa maofisa wa polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Picha Na Hassan Mndeme- Jeshi la Polisi.


No comments: