Kesi ya kwanza ya mteja wa ngono
Mzee mmoa wa miaka 70 aliyepigwa faini ya kroner 13000,- (T.shs.3020897.621) na polisi tarehe 13 Desemba 2009, amegoma kulipa faini. Kugoma kulipa faini kwa mzee huyo kunaweza kusababisha kesi ya kwanza ya mteja wa ununuzi wa huduma za ngono hapa Norway kusikilizwa kwenye kipindi cha majira ya Kiangazi.
Hii itakuwa mara ya kwanza hapa Norway kwa mteja kufunguliwa mashtaka kufuatia sheria ya kukataza ununuzi wa huduma za ngono iliyoanza kutumika Machi Mosi mwaka jana.
Mzee huyo anadai siku aliyokamatwa alikuwa anajiendea zake nyumbani, wala hakuwa na hela mfukoni. Polisi wanadai kuwa, alijaribu kununua huduma za ngono, Strømgaten mjini Bergen. Polisi wanasema kuwa askari kanzu walimfuata mzee huyo alipofuatana na changudoa mmoja kwenye kona za huo mtaa. Huyo mzee na CD hawakuafikiana bei na alipojitokeza kutoka kwenye hizo kona, askari kanzu wakamdaka na kumpiga faini.
Marejeo sheria ya ununuzi wa ngono: seksuallovbrudd
No comments:
Post a Comment