Fikiria mara mbili kabla ya…
Mamlaka ya usalama na uangalizi wa chakula hapa Norway; Norwegian Food Safety Authority (Mattilsynet) wamefunga baaadhi ya maduka ya chakula na mahoteli yanayomilikiwa na wageni hapa Oslo.
Mattilsynet walifanya ukaguzi wa ghafla jana na leo kwenye hizo sehemu na kukuta uchafu wa kusikitisha sana na wa kutia kinyaa…
Wamekuta vyakula viko kwenye sakafu, sakafu zikiwa chafu. Wamekuta nyama zikiwa katika hali ya kuharibika/kuoza, ziko chini kwenye sakafu iliyo chafu, wamekuta mende na panya kwenye baadhi ya mikahawa na maduka na kwenye duka mkahawa mmoja ”Taste of China” wamekuta kuna majiko mawili. Moja la shoo, safi na vifaa vya kisasa. Wakagundua kuna jiko lingine limefichwa, hili ndilo linatumia kupikia vyakula.
Jiko lilikuwa chafu na vyakula vinavyopikwa kwenye jiko hilo havifai kuliwa na binadamu…ukiona jinsi jiko lilivyo na uchafu ulioko kwenye hilo jiko.
Mattilsynet wakaamua kufunga huo mkahawa hapo hapo pamoja na duka moja la kuuza nyama…
Fikiria mara mbili kabla ya kununua vya dezo!
Hawa wamefungiwa. Walikuwa na majiko mawili. Moja la kazi na lingine la danganya toto
Hawa wamepewa onyo.
Hawa wamepewa onyo
Mtaa uliyoko hiyo mikahawa, Torg gata
Duka la nyama limefungwa. Hili limefungwa mara 15 tokea mwaka 1995.
Kila likifungwa, linafunguliwa na mtu mwingine.
Limekuwa likiuza nyama zilizoingizwa Norway kinyemela na
zingine si za kuliwa na binadamu!
Brugata, Oslo.
2 comments:
oh mi nikisema sinunui nyama hapo Brugata watu flani wananiona najifanye highclass.mi nimgeni Norway i didnt know about this stuff lakini ukiingia hapo Butcher,mh u just buy lakini moyoni hujafurahi sana.Nimetumia hiyo butcher not more than 10 times.Siku hizi nanua sehemu flani hivi safiii ila ghaliii(tehe tehe).Mind you sikujua kuhusu hili sakata.Asanteni sana kwa ujumbe .Mwenye masikio na asikie ,tena na wenye macho na waoneee.Tusen takk!
Siku nyingi sanaa mimi niliacha kununua vitu kama nyama na mboga mboga kwenye haya maduka. Naingia kwenye hayo maduka kwa nadra sana..
Sababu kubwa ilikuwa:
Niliingia duka la Zahoor pale Grønland. Nilikuwa na mfuko wangu nimetoka nao duka lingine.
Kwanza:
Nilikuwa mbele ya foleni, jamaa aliyekuwa kaunta, alinipita akiwachukua Wapakistani wenzake.
Pili:
Nilipolalamika nndipo akanihudumia, lakini akataka kuangalia ule mfuko wangu. Nilikataa na kumwambia mbona walionitangulia walikuwa na mifuko hukuiiangalia? Hakuwa na jibu la uhakika.
Tatu:
Kuna vitu vingine wanakuangalia sura kwanza kabla hawagonga bei kwenye mashine ya kaunta.
Nanunua baadhi ya vitu. Nyama na mboga mboga, nanunua siku moja moja kwa shingo upande sana.
Mikahawa ya wageni kama Wachina siingii katu...toka niliposikia wanachanganya nyama na vijinyama vya ajabu ajabu.
Post a Comment