Mtu mdogo kuliko wote afariki.
Mtu mdogo kuliko wote duniani, He Pingping (sentimita 74,6) kutoka Mongolia, amefariki Jumamosi mjini Rome, Italia. He alizaliwa 1988 Wulanchabu, Uchina. Mwaka 2008 alitangazwa rasmi kuwa ni mtu mdogo kuliko wote duniani. Alikuwa nchini Italia akicheza programu kwenye luninga iitwayo ”The Record Show” Mwili wa He utarudishwa alikozaliwa kwa mazishi.
Mwenyezi Mungu Amweke Pema, Amin!
No comments:
Post a Comment