Wednesday, March 17, 2010

Tromsø, Norway

Afungwa siku 16 kwa kuazima pasipoti yake


Mwethiopia mmoja mwenye uraia wa Norway, amehukumiwa kifungo cha siku 16 baada ya kukiri kosa lake la kuazima pasipoti kwa ndugu yake. Jamaa huyo alikuwa likizo kwao Ethiopia, ndugu yake akamwambia kuwa kama anaweza kumwazima pasipoti yake ili kuingilia Sweden. Jamaa aliporudi Tromsø anakoishi, akaituma pasipoti yake kwa ndugu yake huko kwao, kwa kumtumia ndugu yake mwingine kuipeleka.

Huyo nduguye aliitumia hiyo pasipoti kuingia nayo Sweden. Wakati ndugu yake anaingia Sweden, polisi wa uhamiaji wa Sweden walimkamata huyo ndugu yake. Jamaa alipoenda Sweden kuichukua pasipoti yake naye, naye akanaswa.

Chanzo cha habari: Nordlys (Tromsø).

No comments: