Ule wakati umefika
Wiki hii idara ya kodi; skatteetaten (Tax Norway) imeanza kutuma ”selvangivelse/tax return” kwa watu wote wanaoishi Norway. Wiki hii ndipo tutajua kusuka ama kunyoa. Tutajua kama kama tulilipa kodi nyingi na tunarudishiwa hizo hela au tulilipa kidogo na kunapaswa kulipa kodi zaidi serikalini. Kama hujapata barua toka idara ya kodi, unaweza kuingia:
Gateway to the public sector in Norway
Halafu kulia, bofya kwenye mypage..log in to my page via MinID
Hapa unatakiwa kuandika tarakimu zako kumi na moja (personal identity number/fødselsnummer) na nywila uliyokwisha jitengezea. Kama hujafanya hivyo, basi unaweza kujitengenezea nywila (pin code), lakini itachukua kama siku 3 au zaidi kuipata. Au hapo chini ya log in to my page via MinID, unaweza kuoda nywila kwa kuingia:
Order PIN-codes
Kama tayari una nywila, unaiandika, halafu unatakiwa kutumia nywila ulizotumiwa kwenye barua ya tarehe 08.12.2008.
Ukifanikiwa mpaka hapa, basi unaweza kuingia kwenye, sehemu unayopaswa na kuangalia salio lako la kodi, kurudishiwa ama kurudisha.
Wanorwejiani wanasema: lykke til! (Kila la heri)
No comments:
Post a Comment