Monday, March 29, 2010

Volvo yauzwa rasmi kwa Wachina



Kampuni ya Volvo ya magari madogo imeuzwa rasmi tarehe 28.Machi 2010 kwa kampuni ya Geely ya Uchina. Makubaliano hayo ni kati ya Ford ya Marekani iliyokuwa inamiliki Volvo na kampuni ya magari ya Geely ya Uchina, baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Ford na Geely. Zhejiang Geely Holding Group imenunua Volvo kwa Dala za Kimarekani bilioni moja na nukta nane.

No comments: