Friday, March 19, 2010

Wakishaondoka madarakani wanajitia ?
wanademokrasia watakatifu?!




Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


We Frank mpenzi wangu,

Njoo niokoe jamani. Kwa joto la hapa, nakaangwa kama yai, nachomwa kama mbuzi, nachemshwa kama maji na kusongwa kama ugali. Yaani!! Tanuru hili jamani. Kweli ni joto hivi huko uliko? Ndiyo maana inabidi nitafute kazi za hapa na pale kuingia sebuleni wakati bosi au mama bosi wapo (maana kiyoyozi kinazimwa kama wenyewe hawapo na daima hakuna kiyoyozi jikoni au chumbani mwangu). Lakini nikiingia kwa muda mrefu nafukuzwa eti nachelewesha kazi…


No comments: