Thursday, April 01, 2010

Champions League

Arsenal vs. Barcelona 31.03.2010 

9 comments:

Anonymous said...

Tenga na TFF wangemwomba Arsene Wenger kuifundisha Taifa Stars. Anachukua vijana wasio na majina na kuifanya Arsenal timu ya kushindana na timu zote kubwa zeye masupa staa kama Barcelona, Real Madris, Manchester United, Chelsea, AC Milan, Inter, Bayern Munich.

Huyu anaweza kuionoa taifa Stars vizuri mno.

Of coz...litakuja swala la mshahara wake...ni majadiliano tu.

Anonymous said...

WEWE UNA NDOTO ZA ALINACHA..

ARSENAL SIDHANI KAMA WANAWEZA KUMWACHIA HIVI HIVI TU...

PAUNDI ANAZOLIPWA NA ARSENAL...DAU LA KUOTEA MBALI KWA TFF..

LAKINI HATUWEZI KUJUA ANAWEZA KUWA AMECHOKA NA THE GUNNERS NA ANATAKA KUBADILI HALI YA HEWA...

DAR ES SALAAM KUNAMFAA!!!

Anonymous said...

Mie si mpenzi wa the Gunners, lakini soka wanalocheza linanifurahisha kweli ukuchukulia kuwa wastani wa timu ya Arsenal ni miaka 22!!!

Mtambalike said...

Namfananisha Arsene Wenge na Mromania Victor Stansleuas aliyeifundisha yanga miaka ya 1970, jinsi alivyoandikisha vijana pale Jangwani ile miaka na akawajaribu vijana kadhaa (Mimi niki wa mmojawapo...sikuwa kwenye kikosi chake bora)

Jinsi Young Kids ilivyoweza kuwa timu kali na kutoa wachezaji bora wa Yanga na Taifa Stars.

Mnawakumbuka:

1. Juma "Mensah" Pondamali
2. Jaffar Abdulrahman
3. Mohamed Mkweche
5. Saidi Mmanga
6. Mohamed Seugendo
7. Mohamed "Tostao" Yahya
8. Dordian Mapango
9. Kassim Manara
10. Mwarami Mohamed
11. Mohamed "Adolf" Rashad
12. Mohamed Amasha "Mathematician

na wengine nimewasahau...

Hayo yalikuwa matunda ya kocha Victor.

na hivyo ndivyo Arsene Wenge alivyoifanya Arsenal

Mtambalike said...

ni Gordian Mapango

Mtambalike said...

Ahmed Amasha na siyo Mohamed Amasha

Mnazi wa Simba said...

Msiwasahau Simba Kids.

Ilikuwa timu pekee iliyokuwa inawatoa jasho Young Kids

Mtambalike said...

Mara ngapi Simba Kids walikuwa wanafungwa na Young Kids pale uwanja wa kumbukumbu ya Karume. Enzi zile tunaruka ukuta na kuingia bure...

Upo hapo?

Mosi-O-Tunya said...

Eeeh bwana eeeeh!

Enzi zile nazikumbuka za kuruka ukuta pale Karume na pia Neshno Stadium..

Zile zilikuwa enzi za enzi Mtambalike..

Enzi zile zimebaki historia..