Monday, April 12, 2010

Norway

Namba taifa za muda kuchunguzwa.
Waalbania wameharibu!
Karibu Waalbania 500 wanaishi Norway kwa pasipoti za bandia toka nchi za EU (European Union) na ndiyo njia wanayotumia kujipatia manufaa hapa Norway.

Mbinu wanazotumia ni kwenda benki na kufungua akaunti wakiwa na pasipoti batili. Benki nyingi hawana uwezo wa kuangalia kama pasi ni halali au batili. Hivyo wakishafungua akaunti wanapewa namba za muda za taifa zinazoitwa D-Namba. Kabla ya kupewa D-Namba na benki, benki wanatoa kopi ya pasipoti na kuihakiki kuwa ni kopi ya pasipoti.
Jamaa wanatumia hizo kopi zilizohakikiwa kupelekeka kwenye rejesta ya taifa na kuomba namba za kudumu za taifa (National Identity Number/Personnummer). Baada ya hapo wanajitaptia karatasi za kodi na kuweza kufanya kazi bila matatizo. Wengi wameomba mikopo kutoka kwenye mabenki, na wamepotea hawajulikani waliko, na benki nyingi zimepoteza hela kwa namna hiyo.

Jamaa wanaohusika hapa wamejaribu kufuatilia hizo pasipoti walikosema zimetoka, na kukuta hao watu hawapo kwenye hizo nchi.

Benki ambayo imeathirika sana ni DnB NOR na tayari wameshaanza kukataa pasipoti toka nchi nyingi kama ni kitambulisho cha kufungulia akaunti.

Idara ya kodi (skatteetaten) imeanza kushirikiana na idara ya uhamiaji (UDI), polisi na idara nyingine nyeti za serikali, kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa urefu na mapana tatizo la pasipoti za bandia na utoaji wa D-Namba

No comments: