Saturday, April 10, 2010





Sheria mpya ya watoto
hapa Norway - Kuanzia Ijumaa
 9.4.2010 hata kumshika sikio
kumshikisha adabu ni marufuku!


Kuanzia jana Ijumaa 09.04.2010, sheria ya watoto imebadilishwa.  Sheria hiyo itaanza kutumika rasmi Mei Mosi.

Mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha kuwa watoto hawatalelewa kwa aina yotote ya mateso hapa Norway.

Kuanzia sasa sisi wazazi tuwe waangalifu, kwani hata kumshika mtoto kwa kumwonya kwa utovu wa nidhamu ni marufuku!  

Ukionekana unafanya hivyo mbele za watu unaweza kushtakiwa na hata kunyang´anywa mtoto na serikali. Au mtoto mwenyewe akipiga simu sehemu zinazohusika kuwa nateswa na mama na baba, wananifinya masikio nikikosea kitu, basi wazazi wanaweza kushtakiwa hata kunyang´anywa mtoto.

Haishii hapo tu, ina vipengele vingi vingine kwa manufaa ya mtoto (watoto), haswa pale inapokuja suala la wazazi kauchana. Kuanzia sasa, kina baba nao wanapewa nafasi kubwa ya ulezi, baada ya ndoa kuvunjika.

Kipengele hiki cha sheria, kabla hakijapita Bungeni (Stortinget) na kuwa sheria, kimepingwa sana na Wanorwejiani wengi wenye msimamo mkali inapohusu malezi kuwa haiwezekani mtoto afanye atakavyo, bila hata kufundishwa adabu kidogo, lakini serikali iliyopo sasa ya mseto wa vyama vyenye itikadi za siasa za mlengo wa kushoto (vyama vya Kisoshalisti), vimepitisha sheria hiyo kwa vile vina wingi Bungeni.

Ole wetu sisi tuliotoka nchi zenye malezi ya namna hiyo. Tuwe waangalifu sana ama sivyo tutaishia jela au kunyang´anywa watoto au hata vyote viwili



No comments: