Wizara ya ulinzi ya Marekani; Pentagon haitaki watu wasome kitabu hiki kilichoandikwa na luteni kanali Antony Shaffer.
Pentagon imenunua kopi 9500 ya kitabu hiki na kuzichoma moto.
"Pentagon imeamua kununua kopi hizo na kuzichoma moto kwa vile yaliyomo kwenye kitabu hicho yanaweza kuhatarisha ulinzi na usalama wa Marekani" alisema msemaji wa Pentagon, Luteni kanali April Cunningham.
Kwenye toleo la pili la kitabu hiki, baadhi ya majina na taarifa kama 200 zilizokuwepo kwenye toleo la kwanza, zimeondolewa.
Luteni kanali Shaffer alikuwa anaongoza kikosi cha askari maalumu nchini Afghanistan, wakati wa utawala wa Rais George W. Bush
No comments:
Post a Comment