Kijana apigwa risasi kwa kukataa
kupandisha suruali kiunoni!
Jamaa mmoja, Kenneth Bonds (45) mjini Memphis, Tennessee, alishikwa na hasira na ghadhabu na kuamua kumpiga kijana mmoja, Cameron Tucker (17), baada ya Cameron kukataa kupandisha suruali yake kiunoni. Cameron alikuwa amevaa suruali yake, chini ya matako, mtindo unaoitwa ”saggy pants”.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita. Bonds alikuwakuta Cameron na mwenzake Isaac Talyor wakiranda, aliwapigia kelele na kuwaambia wapandishe suruali zao vizuri, wakataa. Akaanza kuwafyatulia risasi, na moja ikampata na kumjeruhi Cameron.
Bonds ameshtakiwa na yuko je kwa mdhamana wa Dala 25.000,- (ishirininatanoelfu)

No comments:
Post a Comment