Thursday, November 04, 2010

Ahadi alizotoa Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika 31 Oktoba 2010


Naamini kuwa Kikwete, iwapo atatangazwa kuwa raisi wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo atakuwa mkweli na kuonyesha heshima kubwa kwa Watanzania wote, waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura kwa kutekeleza ahadi alizozitoa katika kampeni zake. Naamini kwamba ni kutokana na ahadi hizo alizotoa, ndizo ambazo zilimfanya apate kura hizo za kumpa ushindi.

Natumaini kuwa ahadi hizo alizitoa mbele ya Watanzania watu wazima, na wengine wengi wakiwa na umri mkubwa kuliko yeye. Ni adabu na heshima kusema ukweli katika jamii yetu. Atakuwa amewafanyia heshima kubwa Watanzania kwa kutimiza ahadi hizo alizotoa na kwa wakati alioahidi. Wananchi wengi tutakuwa tunafuatilia ahadi hizo kwa umakini sana katika kipindi kijacho. Ahadi hizo ni:

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini

2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga

3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga

4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma

5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini

6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma

7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera

8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera

9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini

10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera

12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera

13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera

14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya

15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera

16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza

18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza

19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita

20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba

21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro

22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini

23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa

24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya

26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga

27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa

28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro

29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini

30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora

31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu

32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini

33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara

34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma

35. Kulinda haki za walemavu- Makete

36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini

37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha

38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora

40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini

41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma

42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini

44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .

45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido

46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro

47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara

48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini

49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa

50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa

51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa

52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda

53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara

54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa

55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar

56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar

57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti

58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma

59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma

60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma

61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma

62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam

63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara

64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha

65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha

66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Mungu Ibariki Tanzania!

Mdau Dingswayo (Jamii Forums)

2 comments:

Anonymous said...

Tuangalie kama hizi ahadi zitatekelezwa au ilikuwa danganya toto!!!!!!!

Anonymous said...

namwonea huruma,kwa sababu hawezi kuzitekeleza na ufisadi kama huuu.I DOUBT IT.