Ahmed Ghailani hana
makosa ya kigaidi!
Mtanzania Ahmed Ghailani aliyekuwa amefungwa Guantanambo Bay kwa tuhuma za kigaidi zilizomhusisha kwa kulipuliwa kwa balozi za Marekani mjini Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998, ameonekana hana makosa ya kigaidi na mahakama moja ya kiraia nchini Marekani. Rais Barack Obama wa Marekani ametaka wafungwa wote waliowekwa kizuizini Guantanamo Bay washtakiwe kwenye mahakama za kiraia ndani ya Marekani. Kwa Ghailani kutoonekana hana makosa ya kigaidi ni pigo kwa serikali ya Obama. Ghailani ni mtuhumiwa kwa kwanza wa makosa ya kigaidi aliyekuwa amewekwa kizuizini Guantanambo Bay, kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia. Ghailani amekutwa na kosa moja tu la kutaka kushiriki kutaka kulipua majengo ambayo ni mali ya Marekani.
Mahakama imesema Ghailani hana makosa ya kigaidi kwa kuwa ushihidi iliotolewa na upande wa mashtaka, ulipatikana kwa njia ya mateso toka kwa shirika la ujasusi la Marekani CIA, hivyo ushahidi huo ni batili na haukubaliki mahakamani. Lakini hataachiliwa toka gerezani kwa kosa hilo la kutaka kuharibu mali ya Marekani. Kwa kosa hilo anaweza kufungwa kati ya miaka 20 hadi kifungo cha maisha.
No comments:
Post a Comment