Friday, November 19, 2010

Chrome ina nyufa nyingi za kiusalama

Orodha ya brauza ”browser” na programu zenye nyufa za kiusalama imetolewa na Google Chrome ndiyo yenye nyufa nyingi zaidi kuliko program zote zilizo kwenye hiyo orodha. Chrome ina nyufa 76 na ni hatari kuitumia kwenye sehemu za kazi kwa ajili ya usalama. Orodha hii imetayarishwa na kampuni moja ya TEKNOHAMA iitwayo bit9 (http://www.bit9.com/ ) imepewa  jina ”2010  Top Vulnerable Applications”

Ifuatayo ni orodha ikianzia na programu yenye nyufa zaidi 
1. Google Chrome (76)
2. Apple Safari (60)
3. Microsoft Office (57)
4. Adobe Reader and Acrobat (54)
5. Mozilla Firefox (51)
6. Sun Java Development Kit (36)
7. Adobe Shockwave Player (35)
8. Microsoft Internet Explorer (32)
9. RealNetworks RealPlayer (14)
10. Apple WebKit (9)
11. Adobe Flash Player (8)
12. Apple QuickTime (6) and Opera (6) - TIE

No comments: