Saturday, November 20, 2010

Haitoshi haki itendeke, lazima idhihirike kweli imetendeka


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

POLE sana mpenzi wangu.  Yaani watu wengine sijui akili zao zikoje!  Au kama anavyosema yule fyatu wako Makengeza, kama akili yako iko katika kulamba miguu ya watu, si inabidi uiname fulutaimu hivyo unachoona ni buti za mabosi tu badala ya hali halisi za watu.  

Yaani  bado siamini kwamba mtendaji kata ambaye ni mtu wa serikali anaweza kuwanyima kituo chenu cha vijana eti kwa kuwa mlifanyia kampeni upinzani. Inamhusu nini?  Kituo kile ni cha chama?  Namkumbuka yule mwalimu aliyetuadhibu sisi sote eti kwa kuwa tulisema hajui kufundisha tunamtaka mwingine.



No comments: